Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yaheshimu faragha mitandaoni-UM

Mataifa yaheshimu faragha mitandaoni-UM

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataiafa kuhusu haki ya faragha, Joseph Cannataci, amelaani sheria ya upekuzi na kuyataka mataifa kote ulimwenguni kuheshimu haki ya faragha ambayo amsema ni haki ya kimataifa katika zama hizi za kidijitali.

Kupitia ripoti yake aliyowasilisha hii leo mjini Geneva Uswisi kwenye baraza la haki za binadamu, Bwana Cannataci ameeleza kusikitishwa kwake kutokana na ukweli kwamba haki ya faragha haihusishwi katika zama za kidijitali, huku akisema kuwa kwa ujumla sheria zimeandaliwa na kupitishwa na nchi mbalimbali ili kuhalalisha matumizi ambayo hayakupaswa kutekelezwa.

Mtaalamu huyo ameenda mbali zaidi na kueleza kuwa haungi mkono sheria ya hivi sasa inayolenga kusimamia upekuzi ambapo amesema kuna ushahidi kidogo au hakuna kabisa wa kumshawishi kuhusu ufanisi au uwiano wa baadhi ya hatua kali zilizowekwa na sheria mpya ya ufuatiliaji katika mataifa ya Marekani Uingereza na Ujerumani na Ufaransa

Amesema anaamini hatua hizo ni za kisiasa na kwamba wanasiasa huzitumia kuonekaan wanafanya kazi, huku pia akiyataka mataifa hayo kukiacha kile alichokiita mchezo wa karata ya haki kwa hofu ya ugaidi na kusisitiza kuimarisha usalama kwa hatau sahihi.