Skip to main content

Kenya na Sudan Kusini elezeni hatma ya raia waliotoweka-UM

Kenya na Sudan Kusini elezeni hatma ya raia waliotoweka-UM

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utoweshwaji wa kulazimishwa, limezitaka serikali za Kenya na Sudan Kusini kuweka hadharani hatma ya wanaume wawili raia wa Sudan Kusini ambao walitekwa nyara na Kenya mwezi uliopita.

Taarifa ya wataalamu hao inasema hakuna tamko lolote kuhusu Dong Samuel Luak, mwanaharakati wa haki za binadamu ambaye alipewa hifadhi nchini Kenya, na Aggrey Idri Ezibon, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya masuala ya kibinadamu ya SPLM upinzani, tangu walipotekwa nyara mjini Nairobi huku wanausalama wakidaiwa kujihusisha .

Ezibon alionekana mara ya mwisho Janauri 24 eneo liitwalo Kilimani mjini Nairobi ilihali Luak alikuwa njiani kupanda basi mnamo Januari 23 kabla ya kutekwa nyara na ndio mara yao ya mwisho kuonekana hadharani. Imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo wataalamu hao wamepongeza hatua ya kusikilizwa kwa shauri hilo na kibali cha hivi karibuni cha kumkamata mtumhumiwa wa utekaji nyara huo ni dalili njema huku wakitaka juhudi zaidi za kiuchunguzi.