Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Houngbo wa Togo awa Rais mpya wa IFAD, aahidi neema mashinani

Houngbo wa Togo awa Rais mpya wa IFAD, aahidi neema mashinani

Waziri Mkuu wa zamani wa Togo Gilbert Fossoun Houngbo, ameteuliwa kuwa Rais wa sita wa mfuko wa kimataifa wa kilimo na maendeleo IFAD, shirika ambalo linawekeza katika kuondoa umasikini katika nchi zinazoendelea duniani.

Taarifa ya IFAD imesema kwamba baada ya uteuzi huo uliofanywa na baraza la utawala la IFAD, Rais huyo mpya anayechukua nafasi ya Kanayo Nwanze anayemaliza kipindi chake cha uongozi, amesema kwa kuwa anatoka mashinani kwahiyo anafahamu vyema madhila ya maeneo hayo,

Mteule huyo anashika nafasi hiyo wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na changamoto ya majanga ya kibinadamu kama vile ya kiasili mathalani migogoro na wakimbizi ilihali nchi kubadili vipaumbele nako kunatishia usitishaji wa kifedha kwa kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Bwana Houngbo kadhalika amenukuliwa akisemani muhimu kulinda matakwa na kuongeza umakini, akisema kuwa IFAD inapaswa kuhakikisha kila dola inayowekezwa itakuwa na thamani kubwa ya fedha