Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO, wadau wajadili usawa wa elimu

UNESCO, wadau wajadili usawa wa elimu

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni,UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu ya Tanzania na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa wameandaa kongamano la siku mbili kuhusu lengo namba nne la maendeleo endelevu SDGs linalohusu usawa katika elimu. Joseph Msami na taarifa kamili.

( TAARIFA YA MSAMI)

Kongamano hilo linalofanyika mjini Dar es salaam linashirikisha nchi 13 za ukanda wa Afrika Mashariki ambapo mawaziri wa elimu wa nchi hizo wanajadili vipaumbele vya kikanda na mapendekezo ya sera kwa ajili ya tafsiri, utekelezaji na ufuatiliaji wa ajenda ya 2010 ya maendeleo endelevu.

Washiriki hao wanafanya mashauriano katika kutayarisha mipango ya baadaye ili kufanikiwa kuandaa dira ya kitaifa ya lengio hilo na kusaidia utekelezaji na ufuatiliaji wa mipango mikakati ya kitaifa, na pia kuorodhesha na kukubiliana na vipaumbele vilivyoainishwa kikanda.

Mashirika wadau waandalizi wa lengo la nne la malengo ya maendeleo endelevu (SDG4) kwa kushirikiana na nchi wanachama 13 wa Afrika Mashariki zinaandaa kongamano la mawaziri la Kanda ya Afrika Mashariki kujadili lengo la nne la malengo ya maendeleo endelevu jijini Dar es Salaam, Tanzania kuanzia tarehe 15 hadi 16 Februari 2017.

Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki Ann Theres Ndon-Jatta amesema.

( Sauti Ann)

''Hii ndiyo maana ya malengo haya lengo ni kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma''