Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufanyia kazi popote kuna faida na changamoto-ILO

Kufanyia kazi popote kuna faida na changamoto-ILO

Ripoti mpya ya pamoja ya Shirika la kazi duniani, ILO na lile la Eurofound, kuhusu teknolojia za kisasa zinazotumika kazini imesema ingawa teknolojia hizo zinazowezesha mtu kufanya kazi za ofisi hata akiwa nyumbani kwake zinaleta ufanisi katika ulimwengu wa kazi, haziheshimu mipaka baina ya kazi na amisha binafsi ya mtu. John Kibego na taarifa kamili

(Taarifa ya Kiebgo)

Ripoti hiyo inasema “Naam”, kupanuka kwa matumizi ya vifaa vya teknolojia ikiwemo simu za rununu za kisasa, tablets na kompyuta umebadili kabisa namna ya utendaji kazi wa kale na kuwezesha ufanyaji wa kazi kubwa kwa muda mfupi, kuokoa muda wa usafiri na hata kuinua kiwango cha uzalishaji.

Hata hivyo, imesema, changamoto ni kwamba zinaweza kusababisha mtu kufanya kazi kwa saa nyingi kwa siku, kufanya kazi kubwa kupita kiasi na kuingilia maisha binafsi ya mtu nyumbani kwke. Jon Messenger kutoka ILO ni mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo

(SAUTI YA JON MESSENGER)

"Kwa sababu mbinu hiii ya kufanya kazi ina faida kwa mfanyakazi aidha mashirika iwapo ina mpangilio sahihi, basi sera zinapaswa kuimarisha faida na kutupilia mbali madhara yake kwa kusisitiza mpango rasmi wa kufanya kazi kutoka sehemu yeyote kwa kutumia intaneti na kudhibiti utendaji kazi usio rasmi au wa muda na pia kuzingatia saa za kazi hususan kufanya kazi kwa muda mrefu ambako kunatajwa kama changamoto."

Ripoti hiyo “Tumika wakati wote, popote pale: Athair zake kwa dunia ya wafanyakazi” imetathimini tafiti zilizofanywa na mashirika hayo katika nchi 15 ikiwemo Ujerumani, Marekani, Japan, Brazil na India ilibaini wajiriwa wengi wa aina mbalimbali wakifanya kazi majumbani kwoa na kwingneko, mbali na mazingira ya kazi zao. Imependekeza kazi hizo zirasimishwe ili wapate nafasi ya kuondolewa kwenye zamu na wafanyakazi nwenzao na kumwepusha kufanya kazi kwa saa nyingi kupita kiasi.