Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania ichukue hatua kwenye matumizi ya mkaa

Tanzania ichukue hatua kwenye matumizi ya mkaa

Hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, Erick Solheim alikuwa ziarani nchini Tanzania kujionea harakati za nchi hizo za uhifadhi wa mazingira na changamoto ambazo inakumbana nazo. Miongoni mwa watu aliokutana nao ni wachuuzi wa mkaa ambapo yaelezwa kuwa biashara hiyo huingizia Tanzania dola bilioni Moja kwa mwaka. Hata hivyo kuna hatua ambazo zilipendekezwa ili kukabiliana na changamoto za biashara ya mkaa kama anavyoeleza Clara Makenya, mratibu wa masuala ya mazingira kwenye shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, alipohojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, Dar es salaam, UNIC.