Vijana Tanzania wachukua mwongozo kwa masuala mbali mbali ya dunia
Kongamano la kimataifa la vijana limeanza leo Jumatatu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa .Mada kuu ya kongamano hilo linalowaleta pamoja viongozi vijana kutoka nchi mbalimbali, viongozi wa serikali, na asasi za kiraia ni jukumu la vijana katika kutokomeza umasikini, na kuchagiza maendeleo katika dunia inayobadilika.
Vijana wanapata fursa ya kujadili na kushauriana mada hizo sanjari na ujumuishaji wa maendeleo endelevu na changamoto kubwa zinazokabili vijana kama ajira.
Ahmad Alhendawi ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu vijana
(ALHENDAWI CUT)
“Umuhi mu wa kongamano hilo la ecosoc la vijana ni kwamba sasa linakwenda sanjari na utekelezaji wa ajenda ya malengo ya maendeleo endelevu, fursa kwa viongozi vijana na nchi wanachama kuja pamoja na kujadili masuala ynayowahusu vijana na utekelezaji wake.”
Naye kijana Peter Siniga ni kiongozi kijana kutoka Tanzania anasema
(SAUTI YA PETER SINIGA)