Vijana Tanzania wajifunza kilichosababisha mauaji ya halaiki

27 Januari 2017

Tarehe 26 Januari mwaka 2017, Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam-UNIC kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ujerumani, Shule za Sekondari, vijana ambao hawapo shuleni na Asasi za kiraia waliadhimisha siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya wahanga wa mauaji ya halaiki, #Holocaust. Shughuli hiyo ilifanyika jijini Dar es salaam, kauli mbiu ikiwa “Kumbukumbu ya mauaji ya halaiki: kuelimisha jamii kwa maisha bora ya baadaye.” Wakati wa shughuli hiyo Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC kilizungumza na wanafunzi na walimu ambao walitoa maoni yao kuhusu kile walichojifunza na matarajio ya baadaye. #Holocaustmemorial

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter