Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yaripotiwa Malakal

Mapigano yaripotiwa Malakal

Milio ya makombora imesikika leo asubuhi katika eneo la Detang, mji wa Malakal kwenye jimbo la Upper Nile karibu na kituo cha ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewaambia waandishi wa habari kuwa ripoti hizo zinafuatia taarifa za mapambano siku ya Jumatano kati ya wanajeshi wa serikali wa SPLA na wale wa upinzani kwenye maeneo ya Detang, Lelo na Bukini.

Hapo jana UNMISS iliripoti kuwa kufuatia mapigano hayo wananchi walikimbia eneo hilo la Detang.

Amenukuu UNMISS ikitaka pande kinzani kusitisha chuki baina yao na kutekeleza kwa ukamilifu mkataba wa amani.