Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yalaani mauaji ya waomba hifadhi wa Kisomali Msumbiji

UNHCR yalaani mauaji ya waomba hifadhi wa Kisomali Msumbiji

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limealaani vikali kitendo cha polisi wa Msumbiji kuwapiga risasi Wasomalia 4 ambao walikuwa wakiomba hifadhi na wameutaka uongozi kuhakikisha waliohusika wanafikishwa mbele ya sheria.

Kwa mujibu wa UNHCR Wasomali hao wanne waliuawa kwa risasi April 29 mjini Namoto jimbo la Cabo Delgado.

Shirika hilo limesema serikali ya Msumbiji lazima iheshimu haki za binadamu za waomba hifadhi na kuhakikisha kitendo kama hicho hakitokei tena. Hata hivyo UNHCR inasema bado inakusanya taarifa zaidi za mauaji hayo.

Msumbiji hivi karibuni imekuwa kivutio kwa Wasomali wanaojaribu kukimbia ghasia na umasikini nchini mwao na kupata usalama na maisha bora tangu mwaka jana.