Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi wa wabunge, Rais utaweka msingi wa ukombozi kwa Somalia

Uchaguzi wa wabunge, Rais utaweka msingi wa ukombozi kwa Somalia

Licha ya changamoto kadhaa zilizokumba uchaguzi ikiwamo rushwa, kwa ujumla uchaguzi wa wabunge nchini Somalia ni nuru njema kwa taifa hilo amesema Michael Keating ambaye ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii, Bwana Keating ambaye leo amelihutubia baraza la usalama leo kuhusu maendeleo ya Somalia, amesema taifa hilo la pembe ya Afrika linatarajia kuwa na uchaguzi wa Rais wa shirikisho, uchaguzi ambao amesema utafungua ukurasa mpya kwani.

(Sauti ya Keating)

‘‘Somalia iankabiliwa na changamoto nyingi na za dharura kama vileukame, pili usalama ambao sio suala la kiufundi tu bali ni makubaliano ya kisiasa  yatakayoimarisha vikosi vya ulinzi na tatu ni kuuwezesha ujumbe wa Afrika Somalia AMISOM, ufanye kazi yake.’’ kudorora kwa hali ya kibinadamu kunakochangiwa na ukame ni changamoto zaidi ya kichumi na kijamii kwa Somalia."

Amesema changamoto ya  ukame inayosababisha kudoroda kwa hali ya kibinadamu, inapaswa kutatuliwa kwa kuimarisha usalama kwani ukame unaathiri wakulima, husababisha ukosefu wa maji na madhila kwa raia takribani milioni tano.