Baridi kali Ulaya yaongeza madhila kwa watoto wakimbizi: UNICEF

Baridi kali Ulaya yaongeza madhila kwa watoto wakimbizi: UNICEF

Ombi limezinduliwa kusaidia maelfu ya wakimbizi na wahamiaji watoto waliokwama kwenye makazi yasiyobora barani Ulaya wakati msimu wa baridi kali ukiendelea.

Takribani vijana 24,000 wamekwama na kujikuta njia panda nchini Ugiriki na nchi za Balkans limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Idadi hiyo inajumuisha watoto wadogo na wachanga wengi kutoka nchini Syria kulikoghubikwa na vita, Iraq na Afghanistan. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva msemaji wa UNICEF Sarah Crowe amesema watoto wadogo wako katika hatari zaidi ya magonjwa na maambukizi.

Amesisitiza kuhusu athari za kisaikolojia kutokana na msongamano na hali duni ya mazingira waliyopo na ametoa wito kwa uongozi kutoa malazi yaliyo bora zaidi.