Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvutano kati ya Palestina na Israel usichochee wimbi la misimamo mikali-Mladenov

Mvutano kati ya Palestina na Israel usichochee wimbi la misimamo mikali-Mladenov

Baraza la usalama leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu hali ya kibinadamu Mashariki ya Kati na hoja ya Palestina. Mjadala huu hufanyika mara kwa mara na huangazia zaidi mgogoro kati ya Palestina na Israel.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati Nickolay Mladenov amehutubia mkutano huo kwa njia ya video kutoka Jerusalem , ambapo amesema licha ya kwamba mgogoro huo una nafuu ukilinganishwa na migogoro mingine katika ukanda huo, tahadhari zaidi inahitajika.

Amesema wadau wote ni muhimu wajizuie na vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga mchakato wa amani.

(Sauti Mladenov)

‘‘Viongozi wa pande zote wana wajibu wa kupunguza mivutano na kuleta nuru ya kisiasa kwa watu wao. La muhimu zaidi ni kwamba wote tuna jukumu la kuzuia mgogoro huu usichochee wimbi la misimamo mikali na udini linalovuma Mashariki ya Kati’