Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa maji mjini watishia sitisho la mapigano Syria

Ukosefu wa maji mjini watishia sitisho la mapigano Syria

Zaidi watu milioni tano wakazi wa mji Damascus, bado hawana maji hatua inayotia uendelevu wa sitisho la mapigano katika eneo la Wadi barada nchini Syria.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa leo mjumbe maalum wa katibu mkuu Umoja wa Mataifa nchiniSyria Staffan de Mistura akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi.

Amesema kuwa anaridhishwa kidogo na habari njema kwamba vijiji vitano katika eneo la Wadi limefikia makubaliano na serikali juu ya maji. Japokuwa vijiji viwili vingine zaidi kile cha Al-Fijah chenye asili ya maji bado hakuna makubaliano na hii inaweza kuleta madhara makubwa na kusababisha mapigano.

Mjumbe huyo amezungumzia juu ya mipango inaendelea juu ya mikutano miwili muhimu ijayo ile itakayofanyika mjini Ankara na Moscow ambapo baadhi ya masuala yatakayojadiliwa ni ukosefu wa maji na mpango madhubuti wa usitishaji wa mapigano. Jambo ambalo laweza kutishia mpangilio wa mazungumzo ya Warusi na Waturuki kushariana na pande kinzani katika mji mkuu wa Kazakh, Astana, Febuari 8.

Mgogoro wa Syria umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miaka mitano sasa na kwa karibu 300,000 wamekufa.