Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AMISOM yahamasisha vijana kushiriki siasa Somalia

AMISOM yahamasisha vijana kushiriki siasa Somalia

Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, umewahamasisha vijana nchini Somalia kushiriki kikamilifu katika siasa, ili kuwa sehemu ya michakato ya uamuzi katika taifa hilo.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa AMISOM, ujumbe huo umeeleza kuwa kupitia kitengo cha masuala ya jinsia, umedhamini taasisi ya vijana SASOYO, ambapo katika mafunzo mkoani Hiiraan, ujumbe huo umeeleza kuwa kujihusisha kwa vijana katika siasa kutaongeza fursa ya nafasi za uongozi kwa kundi hilo.

Mwenyekiti wa SASOYA Bi Naima Ada Elmi amenukuliwa akisema kuwa ikiwa vijana wana malengo ya pamoja na umoja , wanaweza kuleta mabadiliko katika usalama, uchumi na siasa, na kushukuru AMISOM kwa fursa ya kutembelea mikoa na wilaya kwani hatua hiyo imewawezesha kuwahusisha vijana.

Mafunzo hayo yalijikita katika changamoto zainazowakabili vijana na suluhisho, ambapo vijana wameeleza kuwa ukosefu wa ajira unasababisha wengi wao kujiiingiza katika magenge na kukuza kiwango cha uhalifu nchini Somalia.