Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chonde chonde tusisahaulike- UNHCR Uganda

Chonde chonde tusisahaulike- UNHCR Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, nchini Uganda linaomba msaada kwa jumuiya ya kimataifa ili kusongesha usaidizi kwa wakimbizi na wahamiaji kwa mwaka 2017 kwa kuzingatia wimbi kubwa la kundi hilo katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Uganda inahudumia wakimbizi takribani milioni moja wengi wao wakiwa ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Sudan Kusini.

Charles Yaxley ni msemaji wa UNHCR nchini Uganda na katika mahojioano maalum na idhaa hii anataja kile wanachokifanya katika kuhudumia wakimbizi.

(Sauti Charles)

‘‘Wakimbizi wanaofika Uganda wanasaidiwa kwa njia ya kipekee kwa kuwajumuisha kwenye mipango tofauti ya kuweza kufanya kazi ikiwa ni wakulima, wafanyabiashara au madaktari, huu ni mpango ambao umewahamasisha wakimbizi kwenye jamii ambayo ni mfano mzuri wakuigwa barani na ulimwengu kwa ujumla.’’