Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msongo wa mawazo huua, WHO yaasisi kampeni

Msongo wa mawazo huua, WHO yaasisi kampeni

Shirika la afya ulimwenguni WHO limeandaa kampeni kuhusu msongo wa mawazo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuasisiwa kwa shirika hilo yanayofanyika Aprili 7 kila mwaka.

Kupitia chapisho lake WHO inasema msongo wa mawazo unaathiri watu wa kila umri, katika maeneo yote ya maisha, na katika kila nchi huku ukisababisha madhara ya akili, uwezo wa watu kutimiza majukumu yao ya kila siku, huku wakati mwingine ukileta kizungumkuti katika mahusiano ya kifamilia na marafiki.

Msongo wa mawazo pia umeelezwa ma shirika hilo la afya ulimwenguni kuwa husababisha vifo, na twakimu zinaonyesha kuwa hii ni chanzo cha pili cha vifo kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 29

James Chau ambaye ni mwanahabari anaeleza namna msongo wa mawazo uivyoathiri maisha yake tangu akiwa na umri wa miaka mitano.

( Sauti James)

"Kuna wakati nilifikiri kuwa siwezi kuishi hata zaidi ya miaka 25, mambo yalibadilika pale nilipoamua kueleza tatizo na kusikiliza wataalamu wa afya . Jambo muhimu unaloweza kufanya ni kutambua kuwa wewe ni wa muhimu kwa mtu fulani, tafuta mtu wa kuongea naye ,wazazi, marafiki, au yeyote na utakuwa salama."