Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kasi ya usajili wasaka hifadhi Ugiriki iongezeke - UNHCR

Kasi ya usajili wasaka hifadhi Ugiriki iongezeke - UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR leo limerejelea tena wito wake wa kutaka kasi ya usajili wasaka hifadhi kwenye visiwa vya Aegean huko Ugiriki iongezeke ili waweze kuhamishiwa maeneo ya bara. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

UNHCR inasema licha ya jitihada za hivi karibuni za kuboresha mazingira kwenye makazi ya wasaka hifadhi hao, hali bado si shwari kwenye visiwa hivyo vinavyojumuisha Samos, Chios na Lesvos.

Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards amesema hali itakuwa ngumu zaidi mwishoni mwa wiki hii kwani baridi itaongezeka.

Ametolea mfano kisiwa cha Samos ambako watu awapato 700 wakiwemo watoto wako kwenye mahema yasiyo na vifaa vya kuwapatia joto.

Amesema ingawa wadau wamesaidia kuwapatia blanketi bado hiyo haitoshi hivyo wahamishwe maeneo ya bara, jambo ambalo linaweza kufanyika tu usajili unapokamilika.