Umoja wa Mataifa walaani shambulio la kigaidi Istanbul Uturuki.

Umoja wa Mataifa walaani shambulio la kigaidi Istanbul Uturuki.

K

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani shambulio la kigaidi katika klabu ya usiku mjini Istanbul Uturuki, lililotekelezwa wakati wa sherehe za kuupokea mwaka mpya.

Vyombo vya habari vimeripoti kuuawa kwa zaidi ya watu 30 wakiwamo kutoka nchi za nje na kadhaa kujeruhiwa , wakati watu wasiojulikana waliojihami kwa bunduki walipowafyatulia risasi watu waliokuwa wakishereheka na kisha kutokomea.

Katibu Mkuu ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo la kigaidi la mwishoni mwa juma.

Bwana Guterres ameeleza pia mshikamano wake na serikali ya Uturuki na nchi ambazo raia wake waliathiriwa na kuongeza kuwa ana matumaini wapangaji na watekelezaji wa shambulio hilo mjini Istanbul Uturuki watatambuliwa na kufikishwa  katika vyombo vya sheria.

Wakati huo huo baraza la usalama limetoa tamko la kulaani shambulio hilo ililoliita la kikatili.