Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno la wiki-Sasambua

Neno la wiki-Sasambua

Wiki hii tunaangazia neno “Sasambua” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Neno Sasambua lina maana tatu, kwanza ni kutoka na kupanga vilivyopangwa katika sanduku la bibi harusi moja baada ya nyingine. Maana nyingine ni pale mtu anapovua nguo moja baada ya nyingine. Maana ya tatu ni kumporomoshea mtu matusi pasipokuwa na haya wala aibu.