Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo ya Ebola yaonyesha mafanikio: WHO

Chanjo ya Ebola yaonyesha mafanikio: WHO

Chanjo ya majaribio dhidi ya homa kali ya Ebola imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuthibitisha kinga ya hali juu dhidi ya virusi hatari vya ugonjwa huo, kwa mujibu wa chapisho la leo la gazeti la Lancet.

Majaribio yalifanyika Guinea, moja ya nchi iliyoathiriwa kwa asilimia kubwa na Ebola, na chanjo hiyo ni ya kwanza kutoa kinga dhidi ya gonjwa hilo hatari.

Watu zaidi ya 5,000 waliopatiwa chanjo hiyo ya rVSV-ZEBOV huko Guinea hawakupatikana na kisa chochote siku 10 au zaidi baada ya chanjo huku watu 23 ambao hawakupatiwa chanjo hiyo wakipatikana na virusi.

Dkt. Marie-Puale Kleny ni Mkurugenzi msaidizi wa uvumbuzi WHO.

(Sauti ya Dkt. Kleny)

‘‘Sasa tuko katika hatua ambapo mzalishaji anatayarisha waraka, ili kuwasilisha kwa ajili ya usajili , kwa sababu tunachotaka mwishowe ni chanjo ambayo inaweza kutumika bial utafiti.’’