Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi wa bunge dogo waendelea Somalia

Uchaguzi wa bunge dogo waendelea Somalia

Jimbo la South West la Somalia limekamilisha uchaguzi wa viti 69 vya bunge dogo au maarufu kama bunge la wananchi, na kuwa jimbo la pili kufanya hivyo baada ya jimbo la Jubbaland.

Koo zote kubwa tano zimeshiriki upigaji kura jimboni humo ambao umetengewa idadi kubwa ya viti katika bunge la wananchi ikilinganishawa na majimbo yote nchi nzima.

Umoja wa Mataifa na mpango wa Muungano wa Afrika wa kulinda Amani nchini Somalia AMISOM wamekuwa na jukumu muhimu la kuhakikisha mchakato wa uchaguzi katika serikali ya shirikisho unafanikiwa.

Wanawake 14 wameshinda uchaguzi katika bunge dogo jimboni South West, na hivyo kuwapa asilimia 20 ya viti vyote vinavyogembewa.