Tabaka la wafanyakazi Ulaya lazidi kumomonyoka- ILO

23 Novemba 2016

Shirika la kazi duniani ILO limesema tabaka la kazi barani Ulaya linazidi kumomonyoka

Idadi ya watu walio tabaka la kati la wafanyakazi barani Ulaya inazidi kupungua na hivyo kuongeza pengo la usawa na kipato, limesema shirika la kazi duniani, ILO katika ripoti yake ilitolewa leo.

Takwimu katika ripoti hiyo ya ulinganishi inaonyesha kuendelea kupugua tangu kiwango hicho kiporomoke kwa asilimia 2.3 kati ya mwaka 2004 na 2011.

Hali si shwari nchini Ujerumani na Ugiriki ambapo kichocheo kinaelezwa kuwa ni kiwango kidogo cha mishahara kwenye ajira, kupungua kwa idadi ya ajira kwenye sekta ya umma na hata wafanyakazi wa baadhi ya fani kuhamia nchi nyingine kusaka fursa bora.

ILO inapendekeza kuwepo kwa sera bora za ajira na uhusiano bora wa mwajiri na mwajiriwa kama kichocheo cha kuinua tabaka la kati la wafanyakazi, ikitolewa mfano Uholanzi, Sweden na Ufaransa ambako mbinu hizo zimeimarisha uwepo wa tabaka hilo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter