Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukimbizi haujadumaza ubunifu wetu- Wakimbizi

Ukimbizi haujadumaza ubunifu wetu- Wakimbizi

Maisha ya ukimbizini ni ya shida kila uchao. Wakimbizi wakiwa ugenini, hukabiliwa na shida iwe ya mlo, malazi, na hata pengine ubunifu hudumazwa. Lakini baadhi ya wakimbizi wa Syria walioko kwenye kambi ya Za'atari nchini Jordan, wanapishana na simulizi ya aina hiyo, wakiamua kuipa kisogo, na badala yake wake kwa waume kuungana na kuleta ubunifu wake kupitia fasihi simulizi. Je wanafanya nini? Ungana basi na Flora Nducha kwenye makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.