Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumwa na biashara ya utumwa yakumbukwa kimataifa Machi 25

Utumwa na biashara ya utumwa yakumbukwa kimataifa Machi 25

Machi 25 wiki hii ni maadhimisho ya kimataifa ya kumbukumbu ya waathitika wa utumwa na biashara ya utumwa iliyojulikana kama Transatlantic Slave Trade.

Katika maadhimisho hayo Radio ya Umoja wa Mataifa imeamua kuenzi kumbukumbu za mamilioni ya watu ambao waliteseka na kupoteza maisha katika utumwa na biashara ya Transatlantic slave trade.

Inafanya vipindi maalumu katika lugha mbalimbali ikiwemo Kiswahili, ili kutanabahi machungu waliyopitia watumwa, juhudi za kujikomboa na kuwa huru, lakini pia kwa waliosalia wakikumbuka biashara hiyo haramu wamebaki na wosia gani, wamejifunza nini au nini kinapswa kujifunza kutokana na biashara hiyo.

Kwa kifupi biashara ya utumwa ilifanyika kati ya karne ya 15 na 19 ambapo mamilioni ya watu walichukuliwa kwa shuruti kutoka sehemu wakiwemo wanawake, wanaume na watoto na hususani Afrika ya Magharibi ambao walisafirishwa kupitia bahari ya Atlantic hadi marekani kufanya kazi kwenye mashamba ya pamba, wenginge Jamaika kwenye mashamba ya ndizi na hata miwa. Ungana na Flora Nducha kwa undani zaidi

(FEATURE UTUMWA)