Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaongoza msafara wa msaada kwa watoto 15,000 Mosoul

UNICEF yaongoza msafara wa msaada kwa watoto 15,000 Mosoul

Msafara wa msaada unaoongozwa na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na kushirikisha shirika la mpango wa chakula duniani WFP na la idadi ya watu UNFPA umeingia Mosul Iraq kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwli.

UNICEF inasema timu yake inajitahidi kufikisha misaada hiyo ya dharura haraka kwa walengwa na hasa katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na mapigano. Msafarara huo wa magari 14 yakiwemo malori manane ya mizigo yaliyosheheni msaada yamewasili Gogachly Mashariki mwa Mosul asubuhi ya leo.

Malori hayo ymebeba msaada wa kutosha kuwasaidia watoto 15,000 na familia zao ambao ni jumlya ya watu elfu 30 kwa muda wa mwezi mmoja. Msaada huo ni pamoja na paketi 5000 za tembe za kusafisha maji , biskuti za kuongeza nguvu, makopo ya chakula, ndoo, vifaa vya usafi kama sababuni, dawa za mswaki, na vitu vya watoto zikiwemo nepi.

Jumla ya watu 56,000 wakiwemo watoto 27,000 wametawanywa na machafuko Mosoul tangu Oktoba 17 na watu takribani milioni 1.5 bado wamekwama ndani ya mji huo.