Skip to main content

Licha ya mafanikio ya chanjo,surua yaendelea kuua watoto 400 kila siku- UNICEF

Licha ya mafanikio ya chanjo,surua yaendelea kuua watoto 400 kila siku- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema watoto 400 ulimwenguni hufariki dunia kila siku kutokana na Surua licha ya kuwepo kwa vifaa na utaalamu wa kukabili ugonjwa huo.

Kupitia ripoti mpya ya leo, UNICEF imesema licha ya kupungua kwa asilimia 79 kwa vifo vitokanavyo na surua kati ya mwaka 2000 na 2015, bado watoto wanapata ugonjwa huo wenye chanjo.

UNICEF kupitia ripoti ya leo, imesema licha ya kupungua kwa vifo vitokanavyo na surua kati ya mwaka 2000 na 2015, bado watoto wanapata ugonjwa huo wenye chanjo, sababu ikitajwa kuwa ni ukosefu wa utashi wa kisiasa wa kuwezesha kila mtoto kupata chanjo popote alipo.

Dkt. Richard Keezala ni mshauri mwandamizi wa masuala ya afya, UNICEF anasema kile wanachofanya kukwamua hali hiyo..

(Sauti ya Dkt. Keezala)

“Kufanya kazi na serikali katika ngazi ya kitaifa na hata kimkoa na kusaka kutengwa kwa bajeti kutoka serikali kuu au serikali za mkoa ili wapate ili watambue suala la chanjo kwa watoto.”

Amesema kwa upande wake UNICEF..

 (Sauti ya Dkt Kezaala) 

 “Sisi na ubia wa chanjo duniani, GAVI tumepata karibu dola milioni 800 kati ya sasa na mwaka 2025 kwa ajili ya kuboresha utoaji wa chanjo ya Surua, na hii ni hatua chanya na itasaidia karibu nchi 60 zenye kipato cha chini.”