Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya rangi yenye risasi ina hatari za kiafya na kimazingira:UNEP

Matumizi ya rangi yenye risasi ina hatari za kiafya na kimazingira:UNEP

Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP zinaonyesha kuwa rangi zisisizo kuwa na risasi zimetumika katika nchi nyingi kwa miongo kadhaa na zimethibitisha kwamba ni salama na bei yake ni ya chini ilhali ni asilimia 36 pekee yaani mataifa 62 katika ya mataifa 196 ambayo yameweka sheria ya vipimo vya risasi kwenye rangi.

Muungano wa pamoja wa kutokomeza rangi yenye risasi ikiongozwa na UNEP kwa kushirikia na lile la afya duniani WHO limeweka malengo kwa serikali zote kutokomeza matumizi ya risasi kwenye rangi ifikapo mwaka 2020.

Kenya ni moja ya nchi ambako rangi yenye risasi inatumika. Je uelewa wa jamii kuhusu madhara yake ukoje? Ungana na Selina Jerobon kupata hali halisi.