Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi cha maji cha UNMISS chaokoa raia waliozama mto Nile

Kikosi cha maji cha UNMISS chaokoa raia waliozama mto Nile

Kikosi cha maji cha ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Suda Kusini UNMISS, kimefanya uokozi wa watu na mali zao katika mto Nile jimboni Malakal baada ya kuzama kwa boti mbili katika ziwa hilo.

Redio ya UM Sudan Kusini Miraya, imemnukuu Kaimu afisa operesheni wa kikosi cha maji cha Bangladesh Imam Hossain Mohammad, akisema kuwa kikosi cha dharura kilipokea taarifa za kuzama kwa boti hizo na kutapatapa kwa abiria.

(SAUTI MOHAMMAD)

‘Kikosi changu kimefanikiwa kuwanusuru watu kwa kutumia vifaa maalum vya kupiga mbizi, bidhaa kama vile mkaa, mbuzi, na vitu vingine vilipatikana hakuna vifo wala bidhaa zilizopotea.’’

Amewataka wanachi kutoa taarifa muda wowote kuhusu matukio ya majini hususani ya kuzama kwa watu au bidhaa ili kuwezesha operesheni za uokozi .