Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watendaji sahihi ni changamoto: UNMIL

Watendaji sahihi ni changamoto: UNMIL

Wiki ya polisi wa Umoja wa Mataifa imeanza jumatatu ambapo hutumiwa na wanataaluma hao katika kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu operesheni za ulinzi wa amani maeneo mbalimbali duniani.

Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani , wakuu wa vikosi vya polisi kutoka vikosi vya ulinzi wa amani kote duniani wanakutana kujadiliana kuhusu wajibu huo na kujifunza mambo kadhaa.

Katika juma hili, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya polisi UNPOL inaeleza kazi zinazofanywa na vikosi vyake ikiwamo changamoto kama anavyoeleza kamishna wa polisi katika ujumbe wa UM nchini Liberia UNMIL Gregory Hinds.

(SAUTI GREGORY)

‘‘Kuna changamoto nyingi tunazokabiliana nazo. Mojawapo ni watendaji, Kwangu muhimu ni kupata watu wenye ujuzi sahihi, ushindani, maarifa na taaluma. Hili linahitaji mkakati ulioratibiwa vyema kwa kushirikiana na nchi wanachama, na nchi zinazochanngia polisi.’’