Skip to main content

Haiti yaanza kampeni ya chanjo ya kipindupindu-WHO/PAHO

Haiti yaanza kampeni ya chanjo ya kipindupindu-WHO/PAHO

Wizara ya afya ya Haiti leo inazindua kampeni kabambe ya chanjo dhidi ya kipindupindu nchini humo.

Kampeni hiyo inayoanza mjini Les Cayes inafanyika kwa ushirikiano na shirika la afya ulimwenguni WHO na shirika la afya la mataifa ya Amerika PAHO.

Lengo la kampeni hiyo inayoanza leo Jumanne ni kuwachanja watu 820,000 katika wilaya 16 zilizoarifu kuwa na visa au vifo vilivyotokana na mlipuko wa ugonjwa huo.