Skip to main content

Mtoto auawa, walinda amani 32 wajeruhiwa huko Goma, DRC

Mtoto auawa, walinda amani 32 wajeruhiwa huko Goma, DRC

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, mlipuko umeripotiwa leo asubuhi huko Goma, jimbo la Kivu Kaskazini na kusababisha kifo cha mtoto mmoja na walinda amani 32 wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

Radio Okapi ambayo ni kituo cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO imesema kitu kisichofahamika kililipuka majira ya asubuhi kwenye kata ya Keyshero, huko magharibi mwa Goma, wakati walinda amani hao kutoka India walipokuwa kwenye mazoezi yao ya kukimbia ya asubuhi.

Yaelezwa kuwa majeruhi wamepelekwa kwenye kituo cha matibabu cha MONUSCO huku watano kati yao hali zao zikielezwa kuwa ni mbaya.

MONUSCO imewataka wakazi wa eneo hilo la Keyshero kuwa watulivu wakati huu ambapo uchunguzi wa chanzo cha tukio hilo ukiendelea.