Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani mauaji ya raia 26 Ghor:

UNAMA yalaani mauaji ya raia 26 Ghor:

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani vikali shambulio lililofanywa na kundi la watu wenye silaha na kukatili maisha ya watu 26 Jumanne kwenye jimbo la Ghor nchini humo.

Watu whao wenye silaha kwa makusudi waliwapiga risasi na kuwauwa wanaume raia kwenye eneo la Ghalmin wilayani Chaghcharan jimbo la Ghor baada ya kuwashikilia mateka watu hao mapema siku hiyo walipokuwa wakisenya kuni kwenye eneo la Firozokh.

Taarifa zilizopokelewa na UNAMA zinasema watu hao wenye silaha waliwauwa mateka , ili kulipiza kisasi kufuatia kifo cha kamanda wao wakati wa mapigano baiana yao na majeshi ya serikali ya Afghanistan. Pernille Kaedel mwakilishi wa naibu Katibu mkuu na kaimu mkuu wa UNAMA amesema amekarishwa na mauaji hayo ambayo ni ukatili wa kupindukia na kusikitisha, akiongeza kuwa wahusika ni lazima wawajibishwe.

Amesema mauaji ya raia na kuwachukua mateka raia ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa za haki za binadamu na kwamba pande zote katika mzozo wa Afghanistan zinapaswa kuziheshimu.