Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yazidi kusambaratika, Rais atoa wito

ICC yazidi kusambaratika, Rais atoa wito

Wakati idadi ya nchi zilizojitoa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC ikiongezeka na kufikia tatu, Rais wa mahakama hiyo Sidiki Kaba ametoa wito kwa nchi hizo kufikiaria upya uamuzi wao. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Ilianza Burundi, ikafuatia Afrika Kusini na sasa Gambia, nchi hizo za Afrika zikijitoa ICC kwa sababu mbali mbali ikiwemo madai kuwa mahakama hiyo inalenga zaidi Afrika na si kwingineko.

Kufuatia hatua hiyo, Sidiki Kaba, Rais wa baraza la nchi wanachama wa mkataba wa Roma ulioanzisha ICC mwaka 2002, amezungumza na wanahabari huko Dakar, Senegal akitoa wito ya kwamba…

(Sauti ya Sidiki)

“Mosi, nchi wanachama wasake muafaka. Tunakumbuka kuwa mkutano ujao utaanza tarehe 16 hadi 24 Novemba huko The Hague. Pili nchi wanachama waendelee kuwa wanachama na washiriki kwenye kulinda na kutetea maadili ya haki na amani ambayo yalikuwepo kabla ya ICC.”