Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makundi yenye silaha yaachilia watoto 145 Sudan Kusini:UNICEF

Makundi yenye silaha yaachilia watoto 145 Sudan Kusini:UNICEF

Jumla ya watoto 145 wameachiliwa huru leo na makundi yenye silaha nchini Sudan Kusini, limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Hili ni kundi kubwa kabisa la watoto kuachiliwa tangu mwaka 2015, ambapo watoto 1775 waliachiliwa kwenye eneo la Pibor.

Kwa mujibu wa Mahimbo Mdoe mwakilishi wa UNICEF Sudan Kusini, matumaini yao ni kwamba kuachiliwa huku kwa leo kutafuiatiwa na wengine wengi kupata fursa hiyo ili watoto wote 16,000 ambao bado wako mikoni mwa majeshi na makundi yenye sialaha wataweza kurejea nyumbani kwa familia zao.

Wakati wa kuachiliwa kwao na kundi la Cobra na SPLA ya upinzani watoto hao walipokonywa silaha rasmi na kupewa mavazi ya kiraia. Pia wamefanyiwa uchunguzi wa afya na kuorodheshwa katika mpango wa kuwanjumuisha katika jamii.