Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upandaji miti mlima Kilimanjaro kupunguza uhaba wa maji:UNEP

Upandaji miti mlima Kilimanjaro kupunguza uhaba wa maji:UNEP

Mito imeanza kukakuka, ekari zaidi ya 13,00 za misitu kuharibiwa na hofu ya barafu kutoweka katika miongo michache ijayo barani Afrika. Haya ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi limesema shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa mazingira UNEP. Assumpta Massoi na taarifa zaidi

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Ili kulinda mazingira na kuepukana na athari za mabadiliko hayo, ripoti ya UNEP iliyozinduliwa leo nchini Uganda kwenye kongamano kuhusu milima duniani, inasema ni lazima hatua za msingi za upandaji miti zichukuliwekuokoa kizazi cha sasa na kijacho.

Ripoti hiyo “Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ,uhifadhi wa mazingira na mali asili” inasema mfano mlima  Kilimanjaro ulioko nchini Tanzania ni chanzo muhimu cha maji kwa wakazi wa Kilimanjaro lakini pia kujaza mto Pangani ambao husaidia kwa chakula, mafuta na  zana za ujenzi kwa sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki.

Tangu mwaka 1976 miti inaendelea kupungua kwenye  mlima Kilimanjaro, na athari zake sasa zinadhihirishwa na uhaba mkubwa wa maji ambao unawakumba wakazi wa mkoa huo na hususani mji wa Moshi.