Skip to main content

"Vuta uhai”: Uchafuzi wa hewa ni muuaji asiyeoonekana:

"Vuta uhai”: Uchafuzi wa hewa ni muuaji asiyeoonekana:

"Vuta uhai" ni kampeni ya kimataifa inayoongozwa na shirika la afya duniani WHO , muungano wa hali ya hewa na hewa safi, na serikali ya Norway ili kuelimisha kuhusu hatari za kiafya zitokanazo na uchafuzi wa muda mfupi wa mazingira.

Uchafuzi huo unachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la joto duniani na uchafuzi wa hewa. Kampeni hiyo inatilia mkazo maeneo ya kushirikiana elimu baina ya miji, kuongeza kiwango cha ufuatiliaji, kuunga mkono suluhu na kuelimisha watu. Dr Carlos Dora ni mratibu wa WHO kuhusu afya ya umma, afya ya mazingira na jamii.

(SAUTI DR CARLOS DORA)

“Tunazindua kampeni hii ya kimataifa kwa ajili ya hewa safi mijini kwa sababu hewa safi inauhusiano wa moja kwa moja na afya bora, lakini pia kwa mazingira bora na pia sera bora kwa maeneo ya mijini. Kwa sababu kupata hewa safi unahitajji sera endelevu, katika usafiri, katima makazi, katika udhibiti wa utupaji taka katika kilimo mijini, katika nishati kwa ujumla, hivyo kuna usafiri endelevu na sera ambazo zinachangia katika hewa safi, mazingira bora na afya bora.”

Kampeni hiyo pia inasisitiza hatua madhubuti za kisera ambazo miji inaweza kuzitekeleza mfano nyumba bora, usafiri, udhibiti wa taka, na kuboresha mifumo ya nishati.

Pia inachagiza hatua ambazo watu binafsi au jamii zinaweza kuzichukua kama vile kuacha kuchoma taka, kuongeza maeneo ya wazi yanayojali mazingira, na kutembea au kuendesha baiskeli badala ya kutumia magari ili kuboresha hewa .

Vifo takribani milioni 3 kila mwaka vinausishwa na uchafuzi wa hali ya hewa.