Utamaduni kitovu cha ubunifu wa miji: UNESCO

Utamaduni kitovu cha ubunifu wa miji: UNESCO

Ripot mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO inaonyesha kuwa utamaduni ni muhimu katika uhuishaji na ubunifu wa miji.

Ripoti hiyo itakayotolewa na Mkurugenzi Mkuu msaidizi anayeshughulikia utamaduni katika UNESCO Francesco Bandarin, kupitia mkutano wa tatu wa makazi duniani, HABITAT III unaoendelea huko Quito, Ecuador.

Utamaduni unahitaji kuwekwa kikamilifu katika mikakati ya miji ili kuhakikisha mipango endelevu na ubora ya maisha kwa wakazi, inaeleza ripoti hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova ananukuliwa katika ripoti akisema kuwa inatoa ufahamu na ushahidi madhubuti kuonyesha nguvu ya utamaduni katika kujenga miji jumuishi, bunifu na endelevu,.