Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMI yataka mshikamano kwenye operesheni ya Mosul

UNAMI yataka mshikamano kwenye operesheni ya Mosul

Wakati operesheni za kuukomboa mji wa Mosul Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa ISIL au Daesh zikiendelea, mpango wa Umoja wa mataifa nchini Iraq UNAMI umetoa wito kwa raia wa nchi hiyo kushikamana kuunga mkono majeshi ya serikali ambayo pia yametakiwa kuchukua kila hatua kuepuka vifo vya raia.

Ukombozi wa mji wa Mosoul ni operesheni ya Iraq inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, na Umoja wa mataifa unasaidia juhudi za serikali ya Iraq kudhibiti mji wao kutoka mikononi mwa magaidi ili iweze tena kurejesha utawala wa sheria. Mashirika mbalimbali ya Umoja wa mataifa yamekuwa yakitoa msaada kwa jamii kwenye mji huo.