Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi wanategemea misaada nchini Yemen :UM

Watu zaidi wanategemea misaada nchini Yemen :UM

Idadi ya watu wanaohitaji misaada ya kibinadamu kusini mwa Yemen inazidi kuongezeka kutokana na mzozo uliopo ambao umewalazimu maelfu ya watu kukimbia makwao. Hii ni kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo. Kulingana na shirika la kuratibu masuala yakibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA ni kuwa takriban watu 75,000 walilazimika kuhama makwao katika maeneo kadha nchini Yemen.

OCHA inasema kuwa usalama wa raia linasalia kuwa changamoto kubwa wakati mapigano yanapoendelea kuchacha. Ukosefu wa mafuta pia umefanya maisha kuwa magumu hali ambayo imetatiza biashara , utoaji wa hudumu za kiafya na huduma za kibinadamu.