Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umaskini ni zaidi ya kukosa pesa

Umaskini ni zaidi ya kukosa pesa

Tarehe 17 Oktoba kila mwaka ni siku ya kuondoa umaskini duniani, moja ya malengo ya maendeleo endelevu. Umaskini unakwamisha kufanikishwa kwa malengo hayo na ndio maana Umoja wa Mataifa unataka hatua hizo zipatiwe kipaumbele. Nchini Tanzania harakati za kujikwamua kutoka lindi la umaskini nazo zinashika kasi kuanzia ngazi ya kaya hadi kitaifa, huku watu wakiwa na tafsiri tofauti ya neno umaskini. Katika makala hii ya jarida, Nicolaus Ngaiza wa radio washirika Kasibante FM huko Kagera nchini Tanzania alivinjari maeneo mbali mbali kufahamu uelewa wa wananchi na kile wanachofanya kujikwamua.