Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni 41 kufikiwa na kampeni kubwa ya chanjo ya polioBonde la ziwa Chad:UNICEF

Watoto milioni 41 kufikiwa na kampeni kubwa ya chanjo ya polioBonde la ziwa Chad:UNICEF

Kampeni kubwa kabisa ya chanjo inaendelea kwenye bonde la ziwa Chad , kwa lengo la kuwakinga watoto zaidi ya milioni 41 dhidi ya polio, ili kudhibiti mlipuko wa karibuni wa ugonjwa huo Kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF , watu wanaokimbia machafuko katika eneo hilo ndio wanaotia hofu ya virusi vya polio kuweza kusambaa zaidi.

Wahudumu wa afya takribani 39,000 wanapelekwa Nigeria, Chad, Niger, Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ili kutoa chanjo hiyo. Christiophe Boulierac ni msemaji wa UNICEF

(SAUTI YA BOULIERAC)

“Mlipuko wa polio baada ya miaka miwili ya kutokuwepo na visa vyovyote vilivyo ripotiwa inatia wasiwasi mkubwa katika eneo ambako tayari kunashuhudiwa mzozo. Watu wanakimbia mzozo katika eneo hilo na hivyo inazua wasiwasi kwamba huenda virusi vikaenea nje ya mipaka."