Watoaji misaada huko CAR walaani mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wake

27 Septemba 2016

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu, OCHA, huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, imelaani mashambulizi ya nguvu kwa wafanyakazi wa misaada katika mji wa Kaga Bandoro.

Katika mwezi huu wa Septemba, mashambulizi 15 yalitokea ambapo watu wenye silaha walivunja majengo ya shirika moja la kimataifa.

Kutokana na hali hii, OCHA imeshtumu kuzorota kwa ulinzi wa hali ya raia.

OCHA imewakumbusha kwamba unyanyasaji dhidi ya wafanyakazi wa misaada ni uvunjaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu.

Wamesema mashambulizi dhidi ya watoa misaada yanafanyika wakati huu ambapo watu wapatao milioni 2.3 wanahitaji misaada ya kibinadamu huku dola milioni 532 pekee za usaidizi zikiwa ndio zimepatikana.

OCHA imesema licha ya ongezeko la mahitaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, uwekezaji katika hatua za ubinadamu ni muhimu ili kuokoa maisha na kupunguza mateso.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud