Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumewasambaratisha waasi wa mapigano ya wiki iliyopita- MINUSCA

Tumewasambaratisha waasi wa mapigano ya wiki iliyopita- MINUSCA

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA umetoa ripoti kuwa hali katika maeneo ya Ndomete na Kaga Bandoro kwenye wilaya ya Nana-Grébizi nchini humo sasa ni shwari baada ya ghasia ya wiki iliyopita kati ya vikundi vya waasi.

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema MINUSCA inaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu zaidi.

(Sauti ya Farhan)  

"MINUSCA imesema imepata ripoti kutoka serikali za mitaa na wanavijiji kuwa waasi wa Balaka waliokusanyika katika maeneo hayo, wameondoka kutokana na ongezeko la uwepo wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa".

Ameongeza kuwa MINUSCA imesema wapiganaji 4,000 wamesalimisha silaha zao tangu kuanzishwa kwa operesheni hiyo mwezi Oktoba mwaka 2015, operesheni ambayo inatarajiwa kupunguza silaha, kusambaratisha vikundi vya wapiganaji na kuwaunganisha katika jamii.