Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kujadili mabadiliko ya kilimo kukabili mabadiliko ya tabia nchi:FAO

Mkutano kujadili mabadiliko ya kilimo kukabili mabadiliko ya tabia nchi:FAO

Sekta ya kilimo ni lazima ibadilike sio tu kwa ajili ya kupata chakula au uhakika wa lishe bali pia katika kusaidia kushughulikia changamoto zingine za kimataifa kama mabadiliko ya tabia nchi na usugu wa vijiuadudu. Assumpta na Massoi na taarifa kamili

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Hayo yamejitokeza katika Kamati ya kimataifa ya kilimo (COAG) iliyoanza mkutano wake leo Jumatatu kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo FAO mjini Roma Italia.

Mkutano huo utakaoendelea hadi Septemba 30 unajadili masuala mbalimbali ili kusaidia kuhakikisha hatua madhubuti za FAO kwa ajili ya kufanya mabadiliko katika sekta ya kilimo ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Graziano da Silva ni mkurugenzi mkuu wa FAO

(SAUTI YA GRAZIANO)

“ Jukumu la kilimo linakwenda mbali zaidi ya kuzalisha chakula na fedha, mabadiliko ya sekta hiyo lazima yashughulikie mwendeno wa dunia, kama usugua wa vijiwuaduduu, mabadiliko ya tabia nchi, majanga na athari za ukuaji wa miji, vijijini”

Mkutano huo hufanyika kila baada ya miaka miwili kutathimini hali ya kilimo na kutoa muongozo kwa FAO.