Ni jukumu letu kuhakikisha mkutano wa kiamataifa wa kiutu unaleta mabadiliko:Ban
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa viongozi wa dunia , asasi za kiraia na mashirika ya kimataifa kusongesha mbele hatua kubwa za mabadiliko ili kushughulikia ongezeko kubwa na athari za migogoro ya kibinadamu, na kupunguza mahitaji ya kibinadamu , hatari na udhaifu katika miaka ijayo.
Akiwasilisha mkakati wa kufuatilia baada ya mkutano wa kwanza kabisa wa dunia kuhsu usaidizi wa kibinadamu , uliofanyika Mai mwaka huu Uturuki, ametoa wito kwa wote waliohusika kuzingatia ahadi zao na kuzibadili kuwa vitendo vitakavyoleta matokeo mazuri kwa mamilioni ya watu walioathirika na machafuko.

(SAUTI YA PETER THOMSON)
“ Ajenda yam waka 2030 ya maendeleo endelevu inatoa mwongozo kabambe kwa ajili ya mustakhbali wa watu wa dunia hii, na ikitekelezwa ipasavyo italeta suluhu ya muda mrefu inayohitajika ikijumuisha kutokomeza umasikini, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi , na kuchagiza haki za usawa katika mantiki ya kutomsaliza yeyote nyuma.”

Na hatimaye Kamishina wa masuala ya kisiasa kwenye Muungano wa Afrika Bi Aisha Abdullahi akasema changamoto za Afrika zinazopaswa kushughulikiwa kuleta amani ya kudumu na kupunguza janga la kibinadamu.
(SAUTI AISHA ABDULLAHI)
“Mapungufu ya kiutawala na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu , vinasalia kuwa chanzo kikubwa cha migogoro Afrika , na suluhu ni kuboresha taasisi za serikali , kuheshimu haki za binadamu na kutoa usaidizi wa haraka kwa suluhu ya muda mrefu ya ajenda ya maendeleo”
Miradi mipya mbalimbali na ushirika pia vimezinduliwa katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na ule ujulikanao kama Grand Bargain, mkataba mpya wa ubunifu ili kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa fedha na matumizi yake.