Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika kukabili NCD's inahitaji msaada:Kibaki

Afrika kukabili NCD's inahitaji msaada:Kibaki

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amesema amefurahishwa na hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kufanya mkutano muhimu wa wakuu wa nchi na wadau wengine wa afya kujadili maradhi yasiyo ya kuambukiza yaani NCD's.

Akizungmza na mkuu wa Idhaa hii Flora Nducha Rais Kibaki amesema magonjwa ya moyo, saratani, kisukari na yale ya matatizo ya kupumua ni makubwa na kuyatibu ni gharama ambayo watu wengi katika nchi zinazoendela hususani za Afrika kama Kenya haziwezi kumudu.

Ametoa wito wa msaada kutoka nchi tajiri hasa katika upande wa tiba jambo ambalo amesema litasaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu masikini.

(MAHOJIANO NA RAIS KIBAKI)