Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 26 zaahidi dola milioni 151 kwa ajili ya mfuko wa amani wa UM

Nchi 26 zaahidi dola milioni 151 kwa ajili ya mfuko wa amani wa UM

Mfuko wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya ujenzi wa amani, umepigwa jeki ya dola milioni 151 za ahadi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Ahadi hizo zilizotolewa nan chi 26 kwenye mkutano maalumu wa uchangishaji fedha kandoni mwa kikao cha baraza kuu, zitasaidia kwa mwaka 2017-2019 na zitatumika katika miradi mbalimbali katika nchi zaidi ya 20 kwa lengo la kudumisha amani na kuzuia migogoro.

Mkutano huo uliandaliwa na serikali ya Kenya, Mexico, Uholanzi, Jamhuri ya Korea, Somalia, Sri Lanka, Sweden na Uingereza. Na umepokea jumla ya ahadi zinazofikia dola milioni 300 kwa miaka mitatu ijayo.