Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kuzisaidia nchi kupambana na vijidudu sugu mashambani

FAO kuzisaidia nchi kupambana na vijidudu sugu mashambani

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO leo katika mkutano huko Roma Italia limeahidi kusaidia nchi kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto ya kuenea kwa usugu wa dawa za kuua wadudu mashambani. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Shirika hilo limezitaka nchi ziweze kujiandaa kukabiliana na changamoto zinazotokana na dvijidudu sugu au" superbugs " watakapokutana wiki ijayo kwenye mkutano wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa.

FAO inasema, kuenea kwa matumizi mabaya ya dawa za kuua wadudu mashamabani kuna hatari mbaya na husababisha magonjwa sugu kwa binadamu hata mifugo.

Mnamo tarehe 21 september katika kikao maalum cha Umoja wa mataifa , shirika la FAOpamoja na mashirika mengine ya kiamtaifa watatoa kipambele katika kujadidi swala la ongezeko la matumizi mabaya ya dawa za kuua wadudu kwa mimea na mifugo na hatari zake .

FAO imesema itaendelea kushirikia na jamii za wakulima, wafugaji, na mashirika ya uma, katika nchi kama Cambodia, China, Ethiopia, Ghana, kenya,Thailand,Vietnam.