Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 71 cha baraza kuu kitakuwa muhimu sana kwa ajenda za UM:Ban

Kikao cha 71 cha baraza kuu kitakuwa muhimu sana kwa ajenda za UM:Ban

Kikao cha 71 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa kitakuwa muhimu sana, hasa katika kutathimini hatua zilizopigwa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia, lakini pia kuongeza kasi ya utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu.

Akizungumza na wanadishi wa habari mjini New York Ban amesema kikao kijacho kitajikita katika masuala yanayojitokeza , lakini vilevile hali zinazohitaji kupewa kipaumbele zaidi.

Hata hivyo amesema kuna changamoto tatu kubwa, kwanza ni suala la wakimbizi na wahamiaji

(SAUTI YA BAN)

“Jumuiya ya kimataifa ni lazima kushikamana katika moyo wa wajibu wa pamoja kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji duniani. Nchi zaidi lazima zitambue faida za wahamiaji, na kila mtu kila mahali lazima apambane na chuki ambayo wakimbizi wengi, wahamiaji na jamii za wachache wanakabiliana nayo”

Ameongeza kuwa azimio litapitishwa kwenye mkutano wa Jumatatu kuhusu wakimbizi na wahamiaji.

image
Wakimbizi katika kambi ya Daadab nchini Kenya.(Picha:UM/Evan Schneider)
Na suala la pili ni

(SAUTI YA BAN 2)

“Mabadiliko ya tabianchi, nitatumia kila fursa kusukuma kuanza mapema utekelezaji wa mkataba wa Paris kabla ya mwisho wa mwaka huu”

Amesema baada ya mataifa mawili wachafuzi wakubwa wa mazingira Marekani na Uchina kuingia kuridhia mkataba wiki iliyopita , sasa zinahitajika nchi 28 tu ili kupata idadi inayohitajika

image
Mabadiliko ya tabianchi Norwegian Arctic.(Picha:UM/Rick Bajornas)
Na tatu ni masuala ya vitaa mbapo amesema

(SAUTI BAN 3)

“Wakati migogoro mingi inasababisha madhila makubwa , hakuna unaosababisha vifo , uharibifu na hali ya sintofahamu kama vilivyo vita vibaya vya Syria”

Pia amekaribisha usitishaji uhasama wa hivi karibuni na kuchagiza mataifa yenye ushawishi mkubwa kuendelea kutimiza wajibu wao kuepusha adha zaidi kwa watu wa Syria.

image
Katibu Mjuu Ban Ki-moon akitembelea wakimbizi wa Syria walioko kambini Lebanon.(Picha:UM/Mark Garten)
Ban ametaja pia mada zingine zitakazotamalaki kikao cha 21 ni pamoja na afya, uchagizaji wa wafadhili kuchangia kwenye mfuko wa Umoja wa Mataifa, lakini pia yeye kuchukua fursa ya tafakari muongo mziama wa utawala wake , mafanikio na changamoto kabla hajakabidhi kijiti kwa Katibu Mkuu mpya. Kikao hiki cha baraza kuu mwaka huu ndio cha mwisho kwa utawala wa Ban anayetarajiwa kumaliza ngwe yake Desemba 31.